Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa na Naibu Katibu Mkuu wa Tanzania Bara, John Mnyika, wameingia mkoani Tabora kuendelea na vikao vya ndani vya maandalizi ya uchaguzi wa kanda  unaotarajiwa kufanyika Desemba 16 na 17 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tumaini Makene, Amesema kuwa Lowassa na Mnyika wako wilayani Igunga Mkoani Tabora kwaajili ya ujenzi wa chama.

Aidha, amesema Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk. Vincent Mashinji yuko Mkoani Tabora huku Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar Saidi Issa Mohamed akiendelea na vikao vya ndani Mkoani Kigoma akishirikiana na njumbe wa Kamati Kuu Prof. Mwesigwa Baregu.

“Viongozi na wajumbe wa Kamati Kuu na Wabunge wote wametawanyika katika Kanda tofauti tofauti kuimarisha chama”amesema Makene.

Chadema wameamua kutumia mikutano hiyo ya ndani baada ya Rais Magufuli kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na maandamano hadi mwaka 2020.

Mchungaji: Nafahamu kuwa Dettol ni sumu lakini Mungu ameniagiza niwanyweshe
Video: Panga latua wanufaika 'dili' watumishi hewa, Wingu zito kupotea msaidizi wa Mbowe...