Aliyekuwa Mgombea wa urais kupitia vyama vinavyounda Ukawa na Mjumbe wa kamati kuu  Chadema Mh. Edward Lowassa amesema kuwa  uteuzi unaofanywa na serikali ya Tanzania unawabagua vijana kutoka vyama vingine vya siasa.

Akizungumza na vijana leo wa  Baraza la Vijana Chadema katika kikao cha kamati ya utendaji jijini Dar Es Salaam Mh. Lowassa amesema kuwa katika uteuzi ambao unafanya na Rais Magufuli umeegemea upande mmoja na kwamba hauzingatii maslahi ya vijana wote waliopo nchini.

”Ni kweli ajira ni changamoto lakini basi inayopatikana kwanini tusiigawe kwa vijana wote wa CCM, ACT ,CHADEMA na Vyama vingine kwanini wakurugenzi, wakuu wa wilaya na teuzi zingine zinaangalia vijana wa ccm kwani nyie hamjasoma? Alihoji Mh. Lowassa.

Aidha Kiongozi huyo amewataka vijana hao kuwa wamoja kwa kile ambacho wanakifanya ndani ya chama ili kuweza kushika dola kwa mwaka 2020 na kutokubali kuishi kwa migogoro ambayo mingine inatengenezwa na watu.

”Niwaambie mwaka 2020 lazima tushike dola,lakini hatutaweza kushika kama hatutakuwa wamoja, ulimwenguni kote serikali zipo kupinga upinzani na kugombanisha, niwasihii tusikubali kukorogwa”.- Lowassa.

Pamoja na hayo amewasifu vijana hao kwa kukubali  kutii ombi la Mwewnyekiti wa Chadema Taifa kwa kutoenda Dodoma kama jinsi ambavyo walivyokuwa wamepanga hapo awali.

 

Ole Milya Awataka Bavicha Kuenzi Mienendo ya Nyerere na Mandela
Vyuo Vikuu Tanzania Vyatakiwa Kuunga Mkono Uanzishwaji Viwanda