Kiungo mshambuliaji wa Young Africans Deus Kaseke ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inafika tamati msimu huu utakapomalizika

Nyota huyo ambaye alisajiliwa na Young Africans kwa mara ya kwanza mwaka 2015, anawasikilizia mabosi wake ofa ya mkataba mpya

Hata hivyo amesema pamoja na kuwasikilizia viongozi wa klabu hiyo, Kaseke yuko tayari kusikiliza ofa kutoka timu nyingine ambazo zinahitaji huduma yake.

“Bado nina mkataba na Yanga mpaka mwishoni mwa msimu, nasubiri ofa ya mkataba mpya. Kipaumbele nimeipa Yanga lakini hata ikitokea timu nyingine tukafikia makubaliano, sina pingamizi,” amesema

Mpaka wakati ligi inasimama, Kaseke hakuwa na nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Luc Eymael.

Inafahamika Young Africans ipo kwenye mkakati kabambe wa kukisuka upya kikosi chake ambapo nafasi ya washambuliaji wa pembeni ikipewa kipaumbele

Eymael ndiye atakayeamua kama nyota huyo apewe mkataba au la.

Waombolezaji washambuliwa kwa mabomu, 24 wafariki
Visa vya corona vyafika 737, visa vipya 22 vyabainika – Kenya