Kocha mkuu wa Young Africans Luc Eymael amethibitisha kupokea tiketi ya ndege, kwa ajili ya safari ya kurejea Tanzania kuendelea na kazi ya kukinoa kikosi chake.

Eymael amethibitisha taarifa za kupokea tiketi ya safari, baada ya kueleza wazi namna uongozi wa Young Africans ulivyokua umekaa kimya kuhusu mpango wa kumrudisha nchini ili aendelee na kazi.

Kocha huyo amesema amepanga kuanza safari ya kuja nchini Juni 06 ama 07 na atakuwa sehemu ya benchi la ufundi kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya kikosi chake yanayoendelea jijini Dar es salaam.

“Nimeshatumiwa Nimeshapata tiketi yangu ya ndege na nafirikiria mpaka tar 6 ama 7 ya mwezi huu nitakuwa nimeshafika Tanzania kwenye majukumu yangu ya timu.”

“Nikiwasili moja kwa moja nitaanza kazi, ninafahamu kwa sasa msaidizi wangu Mkwasa anafanya kazi nzuri ya kuwanoa vijana, nitakapofika nitaongeza nguvu katika benchi la ufundi na mambo yatakuwa sawa kabla ya kucheza mchezo wetu dhidi ya Mwadui.” Alisema Eymael

Kikosi cha Young Africans kilianza kujiandaa na michezo ya ligi kuu Tanzania Bara (VPL) na Kombe la Shirikisho (ASFC), juma lililopita chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa.

Usiku wa kuamkia jana Jumatano, kocha huyo kutoka Ubelgiji alisema anaushangaa uongozi wa young Africans kwa kushindwa kufanya taratibu mapema kwa kusema Azam FC wameweza kuwarejesha makocha wao nchini lakini kwake hajui kwa nini imeshindikana mpaka Sasa.

“Viongozi wa Yanga wananiambia wameshindwa kunikatia tiketi ya ndege kwenye system, kama wameshindwa kunikatia katika system basi wangenikatia online”

“Ni vizuri kusaini mkataba na La Liga lakini kama unataka kuwa klabu kubwa kwanza jaribu kumrudisha kocha wako haraka iwezekanavyo kama una muheshimu”

Young Africans watarejea dimbani Juni 13 kuendelea na michezo ya ligi kuu dhidi ya Mwadui FC kwenye uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, kisha watapambana na JKT Tanzania Juni 17 mjini Dodoma, Uwanja wa Jamuhuri.

Zahera: Sitaki kuifundisha Township Rollers
Ibrahim Ajib apewa masharti Simba SC