Mshambuliaji  kutoka nchini Hispania Lucas Perez atalazimika kuwa nje ya kikosi cha Arsenal ambacho kesho kitapambana na Sunderland katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England.

Perez atakosa mchezo huo kufuatia majeraha ya kifundo cha mguu alioyapata wakati wa mchezo wa kombe la ligi dhidi ya Reading uliounguruma jumanne usiku kwenye uwanja wa Emirates, na Arsenal walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alipatwa na majeraha hayo kufuatia rafu aliochezewa beki wa Reading Danzell Gravenberch.

Perez tayari ameshaitumiki Arsenal katika michezo mitatu ya ligi ya nchini England na miwili ya kombe la ligi tangu aliposajiliwa mwishoni mwa mwezi Agosti.

Mshambuliaji huyo alijiunga na Arsenal akitokea nchini kwao Hispania alipokua kiitumikia klabu ya Deportivo La Coruna.

Michezo Ya Ligi Kuu 2016/17 Mwishoni Mwa Juma
Sumaye afunguka kuhusu kunyang’anywa shamba, 'CCM wasahau, sirudi Ng’o'