Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kumtumia mshambuliaji Lucas Perez katika kikosi chake cha kwanza ambacho hii leo kitacheza mchezo wa mzunguuko wa tano wa kombe la ligi dhidi ya Reading.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Hispania, amewahi kuanzishwa katika kikosi cha kwanza mara mbili tangu alipojiunga na Arsenal akitokea Deportivo La Coruña mwishoni mwa mwezi Agosti.

Kati kati ya juma lililopita, Perez alicheza mchezo wa ligi ya mbingwa barani Ulaya dhidi ya Ludogorets Razgrad, akiingia kama mchezaji wa akiba katika kipindi cha pili na alisaidia kuchagiza ushindi mnene wa mabao sita kwa sifuri.

“Alifanya mambo makubwa na mazuri wakati wa mchezo wetu na Ludogorets, kwa sababu alitokea benchi na alifanikiwa kuwa katika kiwango cha hali ya juu,” Alisema Wenger, kupitia Arsenal.com.

“Nilimpumzisha kwa makusudi katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita tulipocheza dhidi ya Middlesbrough, kwa sababu nilifahamu jumanne tuna mchezo muhimu dhidi ya Reading.

“Naamini ana mipango mizuri ambayo itamuwezesha kufikia kiwango cha hali ya juu akiwa hapa. Mazoezini ameendelea kuonyesha uthubutu wa kupambana, na kwa kweli ninafurahishwa na kiwango chake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, tayari ameshaifungia Arsenal mabao mawili katika michuano ya kombe la ligi (EFL Cup) walipocheza dhidi ya Nottingham Forest katika mchezo wa mzunguuko wanne, ambapo siku hiyo The Gunners waliibuka kidedea kwa mabao manne kwa sifuri.

Mchina aadhibiwa kwa kuuza bendera ya Zimbabwe
Iker Casillas Apingana Na Waliotoa Habari Zake