Hatimaye kiungo mkabaji kutoka nchini Uruguay na klabu ya Sampdoria ya Italia, Lucas Torreira ameanza safari ya kuelekea jijini London kwa ajili ya kukamilisha mpango wa kujiunga na washika bunduki wa Kaskazini mwa jiji hilo, Arsenal.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya wiki hii, na baadae kutangazwa katika mkutano na waandiahi wa habari, baada ya kukamilisha jukumu la kuitumikia timu ya taifa ya Uruguay kwenye fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini Urusi.

Tayari uongozi wa klabu ya Arsenal umeshafikia makubaliano na klabu ya Sampdoria juu ya uhamisho wa kiungo huyo, lakini pande hizo mbili zilikubaliana mipango ya uhamisho itafanywa baada ya fainali za kombe la dunia.

Kutokana na Uruguay kutolewa katika hatua ya robo fainali, Torreira ameafiki mipango ya uhamisho wake ifanywe katika kipindi hiki ili aweze kupata muda wa kupumzika kwa siku kadhaa, kabla ya kurejea jijini London kuanza mazoezi na wachezaji wenzake watarajiwa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi ya England ambao utaanza rasmi Agosti 11.

Guangzhou Evergrande yamrudisha Paulinho China
Ripoti: Wafanyakazi hulipa kodi zaidi ya waajiri