Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Uholanzi Luciano Narsingh, hii leo anatarajiwa kukamilisha mpango wa kusajiliwa na klabu ya Swansea City akitokea PSV.

Tovuti ya gazeti la Daily Mirror imeripoti kuwa, muda mchache uliopita, mshambuliaji huyo alitua huko mjini Swansea tayari kwa vipimo vya afya.

Usajili wa Narsingh ni sehemu ya mipango ya meneja mpya wa Swansea City Paul Clement, ambaye amepania kuiondoa klabu hiyo mkiani mwa msimamo wa ligi ya nchini England.

Endapo mambo yatakwenda kama yalivyopangwa, usajili wa  Narsingh, utaigharimu Swansea City Pauni milioni 4.

Lipumba aviponda CCM, Chadema
Didi Hamann Aipa Ushindi Man Utd

Comments

comments