Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewataka Makamanda wa Polisi, kusimamia kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kwa kuwalinda wagombea wa baadhi wa vyama vya siasa ambavyo vilitangaza kujitoa, huku wenyewe wakiwa hawajajiondoa kwenye uchaguzi huo.

Waziri ametoa kauli hiyo leo akiwa kwenye maadhimisho ya Miaka 15 ya kifo cha baba yake mzazi, sambamba na leo pia kutangazwa kuanza kwa kampeni nchini.

Ambapo Waziri Lugola  amesema ana taarifa ya baadhi ya watu waliopanga kufanya vurugu, wakati wa kampeni kwa lengo la kuvuruga uchaguzi huo.

Hata hivyo amesema baadhi ya vyama vya siasa vimejitoa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa, lakini wagombea wao hawajajitoa licha ya agizo hilo la viongozi wao kuwalazimisha kujitoa, kwa hatua hiyo kunaweza kukatokea kwa mvutano kati ya makundi hayo.

“Hakutotokea vurugu ya aina yoyote na kabla ya kutokea watakua wameijua na kuishughulikia kwa nguvu zote kuanzia mwanzo wa kampeni, uchaguzi na matokeo yatakapotangazwa”amesema Lugola.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Novemba 18, 2019
Mmarekani mweusi wa kwanza kuwekewa uso bandia

Comments

comments