Wizara ya Mambo ya Ndani imesema kuwa inalaani vikali vitendo vya baadhi ya watu kujichukulia sheria mkononi bila ya sababu yoyote, ikiwemo kupiga, kujeruhi na kupelekea wengine kupoteza maisha.

Hayo yamesemwa Jijini Mwanza na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupita siku chache tokea iliposambaa ‘video clip’ mitandaoni, ikimuonyesha mmoja ya askari mgambo wa jiji akimpiga mwananchi kwa kile kinachodaiwa kutofanya usafi.

“Suala la mgambo waliowekwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwapiga na kuwajeruhi wananchi limewaondolea sifa ya kuendelea kuwatumikia wananchi, ni vyema halmashauri ikatafuta njia mbadala wa kushughulikia suala hilo la usafi na kudhibiti matukio hayo. Hakuna mtu aliyekuwa juu ya sheria nchi hii hivyo tusitoe hukumu na badala yake tuviachie vyombo husika vitimize wajibu wake,”amesema Kangi Lugola

Aidha, Lugola amewataka Watanzania kufuata sheria za nchi zisemavyo na kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.

Hata hivyo, vitendo vya kujichukulia sheria mkononi vimekuwa vikishamili katika miaka ya hivi karibuni, licha ya wanaharakati wengi kuvipigia kelele lakini kumekuwepo baadhi ya kundi wakivipa kipaumbele vitendo hivyo.

 

 

Video: Chadema yapata pigo kuu, Simanzi Monduli
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 3, 2018