Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ameagiza askari mmoja wa kituo cha polisi cha utalii na Diplomasia mjini Arusha kuwekwa mahabusu kwa kushindwa kueleza vitabu muhimu vinavyotakiwa kuwa kwenye chumba cha mashtaka.
“Nimeingia kwenye chumba cha mashtaka, nikamkuta askari nikamuuliza vitabu muhimu kwenye chumba hicho akabaki ameduwaa, nikamuagiza RPC (Kamanda wa Polisi) amuweke ndani. Lakini baadaye nikaamuru atolewe kwani yawezekana askari huyo hana elimu ya masuala ya utalii,” amesema Lugola.
Aidha kituo hiko hakijawahi kutumika tangu kuzinduliwa kwake na askari huyo atakuwa wa kwanza kuswekwa mahabusu humo.
Ni kituo kilichozinduliwa na Rais John Magufuli mapema mwaka huu ambapo tangu wakati huo hakijawahi kupokea mahabusu yeyote. Waziri Lugola, ametoa agizo hilo jana Jumatatu, Julai 23 alipotembelea kituo hicho cha kisasa, ambapo akiwa hapo alimuhoji baadhi ya mambo kadhaa ambayo askari huyo alishindwa kuyajibu kwa ufasaha.

Jose Mourinho amtumia salamu Paul Pogba
DFB wakanusha tuhuma za ubaguzi wa rangi