Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Kangi Lugola amemzuia Kamishna Jenerali wa Magereza, Juma Malewa kuingia kikaoni baada ya kuchelewa.

Tukio hilo limetokea mapema leo Julai 6 dakika chache baada ya kikao hicho cha kimkakati cha viongozi wa vyombo na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kuanza.

Waziri Lugola alisema ikifika saa 5 kamili, mlango ufungwe na kama alivyoagiza ulifungwa, ambapo ilipofika saa 5:1 mlango ulifunguliwa ili Dkt. Malewa aingie.

Alivyoingia, Waziri Lugola alihoji kwa nini Kamishna huyo amefunguliwa mlango, ndipo alimwagiza atoke nje ya kikao kwani alikuwa amechelewa.

Pamoja na Dkt. Malewa kuomba msamaha, Waziri Lugola alikataa na kuonyesha msimamo wake.

Aidha, Waziri Lugola ameagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, kumshusha cheo hadi kubaki na nyota tatu, mkuu wa usalama barabarani, Mbeya (RTO), Leopold Fungu.

Pia ameagiza Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto mkoa wa Kagera, George Mrutu ashushwe cheo.

Msukuma awatahadharisha vijana wa maofisini
Afande Sele ajipanga kumng’oa Sugu Mbeya 2020

Comments

comments