Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amempa wiki mbili Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro kufika ofisini kwake kumueleza mikakati itakayochukuliwa ya kuwawezesha watanzania kufanya kazi kwa masaa 24.

Lugola amesema ili kufikia uchumi wa kati watanzania wanatakiwa kufanya kazi masaa 24 hivyo IGP Sirro anapaswa kumhakikishia mikakati ya jeshi lake katika ushiriki wao kuwapatia watanzania usalama kwa muda wote wakifanya shughuli hizo kiuchumi.

”Nataka IGP aje aniambie kwamba je jeshi la polisi limesalimu amri kwa majambazi ndiyo maana mabasi hayatembei usiku lakini biashara mbalimbali ikifika saa 12 zinafungwa, ukiuliza unaambiwa ni kwa sababu ya usalama nataka IGP aniambie kama majambazi ndio wanaotupatia amri… Hatuwezi kukubali kupewa amri na majambazi ni masaa mangapi tunatakiwa kugafanya shughuli za kiuchumi au kupangiwa maeneo ya kwenda na wapi tusiende”amesema Lugola.

Lugola ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika makao makuu ya kikosi cha kutuliza ghasia kilichopo Ukonga jijini Dar es salaam na kuongea na Askari wa kikosi hicho na wale wanaohudumia katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.

 

Hongera Makonda kwa kupata kidume 'Keagan P Makonda'
Uingereza yadhamiria kombe la dunia 2030