Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kuwa Serikali imeanza yafanyia kazi ipasavyo taarifa za matukio ya watoto kuuawa na kisha kunyofolewa baadhi ya viungo vyao.

Akijibu swali la Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola aliyetaka kusikia tamko la Serikali kuhusu vitendo hivyo vilivyoripotiwa hivi karibuni Mkoani Njombe, Lugola alisema kuwa Naibu Waziri wa wizara yake, Mhandisi Hamad Masauni yuko mkoani humo akifanya kazi na kamati za ulinzi na usalama kudhibiti hali hiyo.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa vitendo hivyo vinatokana na imani za kishirikina zinazowasukuma baadhi ya Watanzania kujiingiza kwenye uhalifu huo.

Aidha, Lugola ametangaza vita dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo hivyo, akiwataka waache kutingisha kiberiti cha Serikali wasije kukipata ‘cha mtema kuni’.

Video: JPM apigilia msumari ma-DC kuwaweka watu ndani, Vyama vya siasa kubanwa fedha za ruzuku

“Lakini taarifa za awali zinaonesha ni imani za kishirikina. Kwahiyo, wabunge watupe ushirikiano kwa sababu Waheshimiwa wabunge maeneo yale wanayafahamu vizuri. Na nitoe onyo, sio kwa Njombe peke yake ila kwa Watanzania wote kwamba wasitingishe kiberiti cha Serikali ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, wasipoacha vitendo hivyo watakipata cha mtema kuni,” alisema.

Waziri huyo aliongeza kuwa tayari wameshapata orodha ya majina ya watu wanaotuhumiwa kujihusha na vitendo hivyo na kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.

Guardiola ainyooshea mikono Liverpool, ‘ni ngumu’
Usalama: Marekani yazihofia Korea Kaskazini, China na Urusi

Comments

comments