Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga (CCM) amezungumzia jinsi alivyopokea kutumbuliwa kwake na Rais John Magufuli ambaye anaamika kuwa rafiki yake akisema hawezi kuhoji uamuzi huo.

Kitwanga aliwaaambia waandishi wa habari nyumbani kwake Misungwi kuwa ingawa hawezi kuhoji uamuzi huo, kuna kundi kubwa la wauza madawa ya kulevya ndio waliolikuza tukio hilo kwa lengo la kumchongea hadi kuondolewa kwenye nafasi hiyo.

“Anayofanya Dk. Magufuli nampongeza sana kwani ni mtu ambaye namfahamu. Ni mwadilifu, msikivu, namshukuru kwa muniamini kufanya kazi naye katika Serikali yake hivyo siwezi kuhoji alichoamua kwa sababau aliyetoa ndiye aliyeondoa,” alisema Kitwanga.

Katika hatua nyingine, Mbunge huyo wa Misungwi alikana kuhusika kwa namna yoyote katika sakata la kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd iliyopewa zabuni ya kufunga mashinde za kutambua alama za vidole kwenye vituo vya polisi nchini, na kudaiwa kulipwa kiasi kikubwa cha fedha wakati kazi haikufanyika kama ilivyotarajiwa. Sakata hilo bado lipo katika uchunguzi japo dalili za kujadiliwa bungeni zinaonekana kufifia.

“Rais wa Kwanza wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Nyerere, kuna wakati alituhumiwa akidaiwa kuwa na mpango wa kumpindua Rais wa Kenya baada ya kuzuru nchini humo. Alipoulizwa na waandishi wa habari alijibu, ‘hivi mtu akikwambia mimi ni mume wa mama yako utakubali?’, sasa hilo ndilo jibu langu kwa Watanzania ili wasiniulize tena,” alisema Kitwanga.

Akizugumzia umiliki wa kampuni ya Infosys, alisema kuwa yeye ni mwanzilishi tu wa kampuni hiyo na hivi sasa inamilikiwa na mwanae baada ya kumuuzia asilimia 33 ya hisa zake na kwamba taarifa ya mauzo hayo ziko wazi.

JPM atuma salamu za rambirambi Mabasi yaliouwa 29, madereva wadaiwa kufanya mzaha
Waziri Mkuu wa Israel atua Afrika Mashariki kwa ziara ya kihistoria, aanza na Uganda