Kocha mpya wa timu ya taifa ya Hispania Luis Enrique leo ijumaa ametangaza kikosi tayari kwa maandalizi ya mchezo wa ligi ya mataifa ya barani Ulaya (UEFA Nations League) utakaowakutanisha dhidi ya England mwishoni mwa juma lijalo, na baadae Croatia.

Luis Enrique ametaja kikosi hicho, huku akionyesha kufuata falsafa ya kuwatumia vijana ambao kwa asilimia kubwa walionyesha kiwango kizuri wakati wa fainali za kombe la dunia 2018.

Katika kikosi hicho, beki wa pembeni wa FC Barcelona Jordi Alba na kiungo wa Atletico Madrid Koke wameachwa na nafasi zao zimechukuliwa na wachezaji ambao hawakuwepo wakati wa fainali za kombe la dunia.

Enrique, anaanza majukumu ya kukiongoza kikosi cha Hispania, huku akiwakosa baadhi ya wachezaji wenye uzoefu kama Andres Iniesta, David Silva na Gerard Pique ambao tayari wameshatangza kustaafu kuitumikia timu ya taifa.

Miongoni mwa wachezaji vijana walioitwa kwenye kikosi hicho kwa mara ya kwanza ni Pau Lopez, Jose Gaya na Dani Ceballos.

Kikosi kamili:

MAKIPA: David de Gea (Manchester United), Kepa Arrizabalaga (Chelsea) na Pau Lopez (Betis)

MABEKI: Dani Carvajal (Real Madrid), Nacho (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Diego Llorente (Real Sociedad), Inigo Martinez (Athletic Club), Jose Gaya (Valencia), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Marcos Alonso (Chelsea) na Raul Albiol (Napoli)

VIUNGO: Sergio Busquets (Barcelona), Sergi Roberto (Barcelona), Rodrigo (Atletico), Saul Niguez (Atletico), Dani Ceballos (Real Madrid) na Thiago Alcantara (Bayern Munich)

WASHAMBULIAJI: Isco (Real Madrid), Marco Asensio (Real Madrid), Diego Costa (Atletico), Rodrigo Moreno (Valencia), Alvaro Morata (Chelsea) na Suso (AC Milan).

Video: Wananchi walia matukio ya walimu kutoa adhabu kali kwa wanafunzi
Makundi ya Europa League 2018/19