Meneja wa klabu bingwa nchini Hispania, FC Barcelona Luis Enrique amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuelekeza lawama kwake na si kwa wachezaji kufuatia kipondo walichokipokea usiku wa kuamkia hii leo.

Enrique ambaye msimu uliopita aliwaongoza FC Barcelona kutwaa ubingwa wa barani Ulaya, ametaka jambo hilo lielekezwe kwake kutokana na baadhi ya mashabiki kuwanyooshea vidole baadhi ya wachezaji wa Barca ambao wanadaiwa hawakucheza katika viwango vyao kama ilivyozoeleka.

Enrique, amesema ana haki ya kulaumiwa kama meneja kutokana na jukumu la kupanga kikosi kilichocheza usiku wa kumkia hii leo dhidi ya Atletico Madrid, lilikua chini yake hivyo haoni sababu ya watu kuzungumza hovyo kwa kuwataja wachezaji.

Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Hispania, amekiri kuumizwa na matokeo ya kufungwa mabao mawili kwa moja, hali ambayo ameichukuliwa kama anguko kubwa kwa msimu huu ambao walijipanga vyema kutetea ubingwa wa barani Ulaya.

“Haikuwa rahisi kukubali kama tumepoteza mchezo, lakini muda ulivyokua unasogea iliniaminisha kweli tumepoteza hivyo nilikubaliana na hali halisi na niliwaambia wachezaji pamoja na maafisa wengine, mimi ndiye napaswa kulaumiwa.” Alisema Enrique

Kikosi cha FC Barcelona, kilikwenda katika uwanja wa ugenini huko mjini Madrid (Vicente Calderón Stadium) wakiwa na ujasiri wa kuongoza mabao mawili kwa moja yaliyopatikana katika mchezo wa mkondo wa kwanza, lakini mpaka dakika 90 zinamalizika, walijikuta wakiloweshwa mabao mawili kwa sifuri.

Atletico Madrid forward Antoine Griezmann is lifted in the air during the celebrations after heading the hosts into the leadAntoine Griezmann akishangulia moja ya mabao aliyoyafunga usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya FC Barcelona

Mabao ya Atletico Madrid katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo, yalifungwa na mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa, Antoine Griezmann katika dakika ya 36 na 88.

Kwa matokeo hayo Atletico Madrid wamesonga mbele kwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa ushindi wa jumla wa mabao matatu kwa mawili.

Klabu nyingine zilizotinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ni Real Madrid, Man City pamoja na FC Bayern Munich.

Young Africans Waendelea Kulia Na Ratiba Ya Kombe La Shirikisho
Antonio Conte Adhamiria Kuvunja Ukuta Wa Real Madrid