Kwa mara ya kwanza meneja wa FC Barcelona, Luis Enrique amezungumzia maamuzi yaliyochukuliwa na mshambuliaji wake kutoka nchini Argentina, Lionel Messi ya kutangaza kustaafiu soka la kimataifa.

Enrique hakuwahi kuzungumza jambo lolote kuhusu hatua hiyo ambayo ilichukuliwa mshambuliaji huyo saa chache baada ya kikosi cha Argentina kupoteza mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya mataifa ya ukanda wa Amerika ya kusini (Copa America) dhidi ya Chile mwezi uliopita.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania, amesema hakushangazwa na maamuzi yalichukuliwa na Lionel Messi, kutokana na kuheshimu na kutambua mchango alioutoa katika upande wa timu ya taifa ya Argentina.

Amesema Messi alifanya maamuzi sahihi tena kwa wakati muafaka na daima ataendelea kumuunga mkono katika jambo hilo ambalo lilionekana kuwashtua mashabiki wengi wa soka duniani kote.

Hata hivyo Enrique, amesisitiza kwamba hata kama itatokea Messi anabadilisha maamuzi na kuamua kurejea kuitumikia timu yake ya taifa, bado atamuunga mkono kwa kuheshimu atakachokifanya.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, alikua miongoni mwa wachezaji wa Argentina waliokosa mikwaju ya penati katika mchezo wa fainali dhidi ya Chile na hatua hiyo inatajwa kuchangia maamuzi aliyoyachukua ya kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa.

Messi alijinasibu kuachana na timu ya taifa ya Argentina kwa kusema anaamini kwake imetosha na haikua bahati yake kupata mafanikio ya kutwaa mataji akiwa na timu hiyo, kama ilivyokua kwa wachezaji waliomtangulia.

Joh Makin Afunguka Kuhusu Kumshirikisha Chidnma Perfect Combo
Jose Mourinho Akataa Kusaini Jezi Za Chelsea