Meneja wa klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelona Luis Enrique, amevitaka vyombo vya habari na baadhi ya mashabiki kuelekeza lawama kwake na sio kwa mtu mwingine yoyote, baada ya kupokea kisago cha mabao manne kwa matatu dhidi ya Celta Vigo katika mchezo uliochezwea usiku wa kuamkia hii leo kwenye uwanja wa Balaidos.

Enrique, ameonyesha kuwa tayari kutupiwa lawama, mara baada ya kukutana na waandishi wa habari ambao walitaka kufahamu sababu ambazo zilipelekea kupoteza kwa kufungwa idadi kubwa ya mabao.

Enrique, alisema anapaswa kulaumiwa kwa matokeo hayo kutokana na kuwa na jukumu la mwisho la nini kilitakiwa kufanyika uwanjani na aliowaagiza walitimiza majukumu yao.

“Mimi ndio mtu wa kwanza ninaepaswa kulaumiwa kwa matokeo tulioyapata hapa ugenini,”

“Tumepoteza wote na tutashinda wote, na jambo la umuhimu ni kuwa mimi ndio huagiza nini kinachotakiwa kufanyika wakati kikosi change kinapokiwa uwanjani kwa lengo la kusaka point tatu muhimu. Ninawajibika kwa kila hatua tuliyoipiga hapa na sitokua mpuuzi wa kukataa lawama.” Alisema Luis Enrique.

Huo unakua mchezo wa pili kwa kikosi cha FC Barcelona kupoteza kwa msimu huu baada ya kufanya hivyo walipocheza dhidi ya Alavés mwanzoni mwa mwezi uliopita kwa kukubali kufungwa mabao mawili kwa moja katika uwanja wa Camp Nou.

Video: Kamanda Sirro aeleza walivyomzima kibaka mtoboa macho
Di Matteo Afungasha Virago Na Kuondoka Villa Park