Aliyekua Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Luis Miquissone amesema ataendelea kuwa Mwanafamilia wa klabu hiyo kutokana na mambo mema aliyofanyiwa na mabingwa hao.

Miquissone aliondoka Simba SC miezi miwiwli iliyopita, akisajiliwa na Mabingwa wa Soka Barani Afrika Al Ahly ya Misri kwa ada iliyofanywa siri baina ya pande hizo mbili.

Kiungo huyo kutoka nchini Msumbiji amesema Simba SC walimpokea na kuishi vizuri katika klabu hiyo na muhimu zaidi alipewa nafasi ya kuonyesha kipaji chake, akaaminiwa na kuwa kipenzi cha mashabiki.

“Niliondoka kwa amani, vongozi walinipa baraka zote kwahiyo Simba kwangu ni kama familia iliyonilea vizuri sana. Niliflka pale nikiwa na kipaji lakini sikuwa na jina kubwa, Waliniamini wakanipa nafasi nikaonyesha nilichonacho. Naweza sema kwangu walikuwa walezi bora”

“Unajua Simba ni timu kubwa sana kwenye ukanda ule wa CECAFA kwahiyo ukicheza Simba na wakakuamini ni jambo la kujivunia. Simba ndiyo timu niliyoichezea kwa mafanikio Wamenifanya Nicheze Hatua ya Makundi na Robo Fainal ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ‘Caf Champions League’. Sikuwa nimecheza kabla kwa hiyo walinipa kitu kipya kwenye maisha yangu ya soka.”

“Kuhusu pengo langu kuzibika pale inawezekana tu kwa sababu mimi sio mchezaji bora wa Muda wote pale Simba ina maana kuna watu walipita na mimi nilipoenda nikaziba nafasi zao, kwa hiyo naamini kama walikuwa na jicho la kuniona mimi na kunisajili basi mpaka sasa washasajili mchezaji wa kuziba pengo langu na huwenda akatimiza majukumu ya Simba vizuri kuliko hata mimi.”

“Simba SC ni familia yangu na najua mashabiki wananipenda sana, ikitokea nafasi ya kurudi pasipo na shaka niterejea. Naamini ipo siku.” alisema Miquissone

Habari Picha: kilele mbio za mwenge
Mr Tanzania kutafutwa Octoba 22, 2021