Mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona Luis Suarez, amesema bado klabu ya Liverpool itaendelea kuwa muhimu maishani mwake, kutokana na mambo makubwa aliofanyiwa akiwa Anfield.

Suarez aliitumikia Liverpool kwa miaka mitatu na nusu na kupata mafanikio ya kuwa mfungaji bora katika ligi ya nchini England, msimu mmoja kabla ya kutimkia FC Barcelona.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Uruguay, amezungumza maneno hayo kufuatia mchezo wa kirafiki ambao utazikutanisha klabu hizo mwishoni mwa juma hili katika uwanja wa Wembley uliopo jijini London.

“Bado klabu hii inaendelea kuwa kumbukumbu kwangu, kutokana na maisha mazuri niliyoyapata Anfield, daina sitoisahau na nitaendelea kuienzi katika maisha yangu yote,” Suarez alikaririwa na tovuti ya Liverpoolfc.com.

“Ni faraja kucheza mbele ya mashabiki wa Liverpool kwa zaidi ya miaka miwili, tena ikafikia hatua wakakubaliana na mchango ulioutoa, hivyo kwangu sitochoka kuipenda na nitaendelea kusema jambo hili hadi mwisho wa maisha yangu.

Liverpool watacheza na FC Barcelona mwishoni mwa juma hili, ikiwa ni muendelezo wa michezo ya michuano ya mabingwa wa kimataifa (International Champions Cup), ambayo inatumika kwa ajili ya kujiandaa na msimu wa 2016/17.

Real Madrid Kumpandishia Mshahara Zinedine Zidane
Fernando Llorente Kutimkia Liberty Stadium