Mshambuliaji kutoka nchini Uruguay na klabu ya Atletico Madrid ya Hispania Luis Suarez, huenda akarejea nchini England kujiunga na klabu ya Aston Villa inayonolewa na Steven Gerrard.

Suarez aliwahi kucheza na Steven Gerrard wakiwa na kikosi cha Liverpool, na ukaribu wao unatajwa kuwa kichocheo cha Mshambuliaji huyo kutamani kurejea nchini England.

Mkataba wa Suarez na Atletico Madrid unatarajiwa kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu, hivyo huenda akaelekea Villa Park kama mchezaji huru.

Tayari Klabu ya Aston Villa imemsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Philippe Coutinho ambaye pia aliwahi kucheza sambamba na Gerrard, wakiwa Liverpool.

Endapo dili hili likifanikiwa, Villa watakuwa na kikosi imara zaidi, kwani mbali na Surez, wachezaji wengine wanaotajwa kuwaniwa na klabu hiyo ni Digne, Watkins na Buendia.

Waziri Ndaki atoa maelekeezo kwa wakusanya maduhuli ya serikali
Vlahovic aikataa Arsenal, kusajiliwa Juventus