Mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona, Luis Suarez atakua nje ya uwanja kwa muda wa majuma mawiili, kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya goti.

Mshambuliaji huyo alipatwa na maumivu wa goti wakati wa mchezo wa ligi ya Hispania mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Atletico Madrid uliomalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Mwanasoka huyo kutoka nchini Uruguay ameachwa kwenye safari ya nchini Uholanzi, ambapo kikosi cha FC Barcelona kesho Jumatano kitakua na shughuli kubwa ya kuwakabili PSV Eindhoven, katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Suarez anaungana na Sergi Roberto, anayekabiliwa na majeraha misuli ya paja, ambayo yatamuweka nje kwa muda wa majuma matatu.

Naye kiungo Rafinha Alcantara ataendelea kuwa nje ya uwanja hadi mwishoni mwa msimu huu, kufuatia majeraha ya goti alioyapata akiwa katika mchezo dhidi ya Atletico Madrid uliounguruma Wanda Metropolitano, mjini Madrid.

Kiungo kutoka nchini Brazil Arthur pia ameondolewa kikosini kwa sababu za kuwa na majeraha ya goti, lakini viungo Ivan Rakitic na Philippe Coutinho wamerejea kikosini.

Baba amuua kijana aliyemkuta na binti yake aliyepotea
Gianluca Vialli: Nipo Vizuri japo siijui kesho yangu

Comments

comments