Mshambuliaji kutoka nchini Uruguay na klabu ya Barcelona, Luis Alberto Suárez Díaz, amesema hana cha kujutia kwa kushindwa kujiunga na Arsenal wakati alipokuwa akiitumikia klabu ya Liverpool.

Wakati wa majira ya kiangazi mwaka 2013, Arsenal walituma ofa ya kuhitaji saini ya Suarez lakini meneja wa klabu ya Liverpool, kwa wakati huo Brendan Rodgers, alikataa kumuuza mshambuliaji huyo ambaye alikua moto wa kuotea mbali akiwa na The reds.

Katika msimu huo, Suarez alipata mafanikio makubwa kwa kufunga mabao 31 na kuifanya Liverpool ikaribie kutwaa ubingwa wa michuano ya ligi kuu ya soka nchini England, lakini ilizidiwa kete katika michezo ya mwisho.

Rodgers and Suarez

Baada ya kupata mafanikio hayo, Suarez mwenye umri wa miaka 29, alikwenda kujiunga na FC Barcelona na ameshatoa mchango mkubwa ulioiwezesha klabu hiyo ya Camp Nou kutwaa mataji matatu ya Ligi ya La Liga, Klabu Bingwa Ulaya na Kombe la Kopa del Rey msimu uliopita.

Akiwa kaskazini mwa jijini London yalipo makao makuu ya klabu ya Arsenal, kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora, usiku wa kuamkia leo, Suarez aliwaambia waandishi wa habari haoni cha kujutia kwa kutosajiliwa na meneja  Arsene Wenger.

“Arsenal ni klabu kubwa, lakini ingekuwa vigumu kucheza klabu nyingine nchini Uingereza zaidi ya Liverpool,” alisisitiza Suarez

Alisema kwamba Barcelona ndio lilikuwa chaguo bora kwake, licha ya kufanikiwa kutwaa mataji matatu katika msimu wake wa kwanza, lakini familia yake inafurahi kuishi katika mji huo huku akiongeza kuwa Barca hiyo ndio chaguo lake pekee kwake na maisha yanakwenda vizuri.

Kampuni Ya Adidas Yafanywa Chambo Wa Kumnasa Paul Pogba
Azam FC Kuweka Kambi Nje Ya Nchi