Chama cha Wafanyakazi  nchini Brazili kimemteua aliyekuwa rais wa nchi hiyo ambaye amefungwa jela kwa makosa ya rushwa, Luiz Da Silva kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Kwa mujibu wa mtandao wa US. News wa nchini Marekani,  umeripoti kuwa Wajumbe wa chama hicho walithibitisha kuwa Da Silva aliyekuwa rais katika kipindi cha mwaka 2003 na 2010 atagombea tena kiti hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Aidha, mtandao huo umeripoti kuwa, rais huyo wa zamani huenda akazuiliwa na mahakama ya uchaguzi nchini humo, kugombea tena kiti hicho.

Hata hivyo, tangu mwezi Aprili, 2018, Da Silva yuko gerezani akitumikia kifungo chake kutokana na kosa la kula rushwa, ingawa yeye mwenyewe anakana kosa hilo akisema kuwa limechagizwa na kisiasa.

Mbunge awalipia ada wanafunzi kidato cha tano na sita
Moise Katumbi amkalia kooni Rais Kabila