Klabu ya Real Madrid, imethibitisha kuumia kwa kiungo wao kutoka nchini Croatia, Luka Modric ambaye ameonekana kuwa muhimili mkubwa kwenye kikosi cha Rafael Benitez kwa msimu huu.

Real Madrid wamethibitisha taarifa hizo, baada ya siku moja kupita ambapo ilishuhudiwa Modric akipata majeraha ya paja akiwa na timu ya taifa lake, wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za barani Ulaya za mwaka 2016 dhidi ya Bulgaria.

The Meringues, wamechelewa kuthibitisha kuumia kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30, kutokana na mawasilino ambayo yalikua yakiendelea kati yao na shirikisho la soka nchini Croatia.

Modric, alilazimika kuondolewa kikosini wakati mchezo dhidi ya Ubelgiji, baada ya kipindi cha kwanza, kutokana na malalamiko aliyo yawasilisha kwa daktari wa timu kuhusu maumivu ya paja aliyokua akiyahisi.

Hata hivyo jana mchana Modric, alisafiri kuelekea mjini Madrid kwa ajili ya kufanyia vipimo kwa mara ya pili na ilibainika kweli anasumbuliwa na tatizo hilo.

Kwa mantiki hiyo sasa, Modric ataukosa mchezo wa ligi ya nchini Hispania, utakaochezwa mwishoni mwa juma hili ambapo Real Madrid watapambana na Levante.

Kuelekea Ufaransa 2016, UEFA Watoa Utaratibu
FA Yamuadhibu Tena Jose Mourinho