Mshambuliaji mpya wa Manchester United, Romelu Lukaku ameanza vema kutimiza ndoto yake ya kuichezea timu hiyo kwa kufunga magoli mawili katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya  West Ham United.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye magoli yake mawili yalikamilisha ushindi wa mabao manne dhidi ya West Ham, amesema kuitumikia United ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu iliyotimia.

Lukaku ni mmoja kati ya wachezaji watatu wakutumainiwa waliosajiliwa katika msimu wa majira ya joto akitokea katika klabu ya Everton kwa dau la  paundi million £75m.

Akizungumza na Sky Sports News, mchezaji huyo amesema ana furaha kuwa sehemu ya Mashetani Wekundu.

“Kucheza mbele ya mashabiki wa aina hii ni ndoto ambayo imekuwa kweli lakini muhimu zaidi ni pointi tatu. Na kuchezea Manchester United unakuwa na kazi ya kufanya na kazi yangu ni kufunga magoli,” ameema Lukaku.

Lukaku amekuwa mmoja kati ya wachezaji wanne kufunga magoli mawili katika mchezo wa ufungizi wa ligi kuu ya Uingereza iliyoanza wikiendi hii, wachezaji wengine walio funga magoli mawili kila mmoja ni pamoja na Sam Vokes (Burnley), Steve Mounie (Huddersfield Town ) na Jamie Vardy (Leicester City).

LIVE: Rais wa Misri awasili Tanzania
Sakata la Escrow lazidi kuwatafuna vigogo, sasa latua kimataifa