Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku amekana makosa ya kupiga kelele katika nyumba aliyokuwa akiishi baada ya kukamatwa nchini Marekani mapema mwaka huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alishtakiwa kwa makosa hayo mnamo mwezi Julai baada ya maafisa wa Polisi kupata malalamiko ya kelele katika nyumba moja huko Los Angeles.

Raia huyo wa Ubelgiji hakuwasili mahakamani katika mji wa Los Angeles siku ya Jumatatu na wakili wake Robert Humphreys aliwasilisha mahakamani ombi la mchezaji huyo kutokuwa na makosa hayo ambapo Kamishna Jane Godfrey alihairisha kesi hiyo.

Baada ya kesi hiyo kusikilizwa tena wakili James Eckart alisema kuwa iwapo mshambuliaji huyo atapatikana na hatia atakabiliwa na faini na kulipa gharama za fedha zilizotumika kupiga simu kwa siku tano.

Lukaku ambaye yupo katika kiwango kizuri alilipotiwa kupata maumivu Jumamosi iliyopita wakati United ilipocheza dhidi ya Crystal Palace jambo ambalo lingemfanya kukosa mchezo wa timu yake ya taifa ya Ubelgiji dhidi ya Bosnia. lakini baada ya kufanyiwa vipimo imegundulika kuwa hana tatizo kubwa.

 

Mkuu wa Mkoa Tanga ajifananisha na Makonda
Yanga kumkosa Ngoma kwa wiki moja