Mshambuliaji wa klabu ya Everton Romelu Lukaku bado anawazunguusha akili viongozi wa klabu hiyo, kutokana na kuonyesha hana haraka na mpango wa kusaini mkataba mpya.

Gazeti la The Sun limeeleza kuwa, tayari uongozi wa Everton umeshamuwekea mezani mshambuliaji huyo mkataba mpya ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni 135,000 kwa juma, lakini hakuna kinachoendelea mpaka hivi sasa.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa Lukaku ameliacha suala la mazungumzo ya mkataba mpya mikononi mwa wakala wake Mino Raiola, kwa kuamini muda uliopo ni wa kucheza soka na sio kuingia katika mijadala ya mambo mengine.

Wakati maamuzi hayo yakichukuliwa na Lukaku, tetesi za vyombo vya habari nchini Ujerumani pamoja na England zinatabaisha kwamba klabu za FC Bayern Munich na Chelsea zipo katika mawindo ya kumsajili mshambuliaji huyo kutoka nchini Ubelgiji.

El-Maamry Kukutana Na Simba, Young Africans Novemba 3
Lowassa ahudhuria Kikao cha Bunge kama mgeni