Mshambuliaji wa klabu ya Everton Romelu Lukaku, anaamini kiungo wa Man Utd Paul Pogba huenda akawa mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2016.

Lukaku amethibitisha imani hiyo, kwa kusema wazi aliwahi kumwambia Pogba kuhusu uwezekano wa kutwaa tuzo ya mchezaji bora duniani, na kumaliza kasumba iliyokithiri katika miaka ya hivi karibuni kwa tuzo hiyo kuchukuliwana Lionel Messi ama Cristiano Ronaldo.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha SFR Sport, Lukaku amesema anaridhishwa na uwezo wa kiungo huyo kutoka nchini Ufaransa, na kwa sasa haoni wa kumuweka pembeni katika harakati za kutangazwa kuwa mshindi.

“Pogba anaweza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or)? Aliulizwa Lukaku, akajibu “ndio”.

“Anajua nini cha kufanya anapokua uwanjani hivyo sina shaka na imani yangu dhidi ya Pogba,”

“Sijali kwa namna watu wanavyomchukulia Pogba, najua wapo baadhi wanamuona ni wa kawaida na wengine wataungana na mimi kuthibitisha ubora wake, lakini bado nasisitiza Pogba ana nafasi kubwa ya kuibuka kinara kwa 2016.” Alisema Lukaku.

Gareth Southgate Kumpa Mtihani Harry Kane
Super Mario Amuita Mamadou Sakho Ufaransa