Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki, Lukas Podolski ameondolewa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Ujerumani kufuatia jeraha ya kifundo cha mguu.

Ujerumani wameweka kambi ya kujiandaa na michezo ya kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya, dhidi ya Ireland pamoja na Georgia.

Podolski, alijiunga na wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani siku ya jumatatu, na jana alifanyiwa vipimo na kubainika ana tatizo katika kifundo cha mguu wake wa kulia.

Taarifa kutoka shirikisho la soka nchini Ujerumani zinaeleza kwamba, mshambuliaji huyo ameruhusiwa kuondoka na kurejea nchini Uturuki, kwenye klabu yake kwa ajili ya kuendelea na matibabu.

Wakati Podolski akiondoka kambini, kiungo wa klabu ya Bayer Leverkusen, Karim Bellarabi ameendelea kufanyiwa matibabu ya bega na imedhihihir atakuwa na uwezo wa kucheza mchezo wa siku ya Al-khamis dhidi ya Ireland utakaochezwa mjini Dublin, na kisha watarejea nyumbani kupambana na Georgia katika mji wa Leipzig mwishoni mwa juma hili.

Wachezaji wengine waliokua tayari kupambana hiyo kesho ni Marco Reus, Mario Goetze pamoja na Andre Schuerrle ambao walimaliza michezo ya ligi ya mwishoni mwa juma lililopita kwa mashaka kutokana na majeraha madogo yaliyowakumba.

Magufuli Atua Kwa Lowassa, Amwaga Ahadi
Gerd MĂĽller Bomber Asumbuliwa Na Alzheimer