Klabu ya Man Utd imethibitisha taarifa za Luke Shaw kufanyia upasuaji akiwa nchini Uholanzi baada ya kuvunjika mguu kwenye mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi, kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya usiku wa kuamkia jana.

Man Utd imeeleza kwamba, beki huyo mwenye umri wa miaka 20, alilazimika kuachwa nchini Uholanzi kwa matibabu na tayari amefanyiwa upasuaji kwa mafanikio makubwa.

Taarifa zinaeleza kwamba Shaw ataendelea kubaki mjini Eindhoven kwa matibabu mpaka hapo atakaporuhusiwa kurejea nchini England, na kuendelea na mapumziko ya kuuguza jeraha la mguu wake wa kulia.

Kabla ya taarifa za klabu kutolewa kupitia tovuti maalum, meneja Louis Van Gaal alinukuliwa na vyombo vya habari akisema Luke Shaw alipangiwa kurejea nchini England kwa ajili ya ufanyiwa taratibu zote za matibabu yake.

Kutokana na ukumbwa wa jeraha la Luke Shaw, inahisiwa huenda beki huyo akawa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi sita ijayo.

Pacquiao: Akirudi Poa, Asiporudi Poa
Magufuli Afunika Kigoma, Angalia Video