Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuwakamata baadhi ya maafisa ardhi na baadhi ya wanasheria ambao wamehusika katika uuzaji wa shamba kiasi cha Hekta mbili na nusu mali ya Madina Omary Mkazi wa Bagamoyo mkoani Pwani.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma wakati akimrejeshea mama huyo ardhi yake huku akiwataka maafisa ardhi na wanasheria kufuata taratibu zote za uuzaji wa ardhi wakati wa kuuza.

Amesema kuwa uuzaji wa shamba hilo ulikiuka taratibu za uuzaji wa eneo hilo ikiwemo kuwepo kwa sahihi za kufoji za wahusika wa shamba hilo huku mawikili waliofanya hivyo wakijua kuwa hilo ni kosa kisheria.

Hata hivyo, kwa upande wake mmliki wa eneo hilo, Madina Omary amemshukuru Lukuvi kwa kumsaidia kupata ardhi hiyo ambayo alikua amedhulumiwa kwa zaidi ya miaka kumi kutoka kwa matapeli ambao alikua akishindana nao mahakamani.

Rais Buhari aunga mkono kufukuzwa kwa Walimu 20,000
Video: Italy yashindwa kufuzu kombe la dunia 2018