Waziri wa Ardhi William Lukuvi amekabidhi ekari 715 za ardhi kwa manispaa ya kigamboni kama ilivyoagizwa na Rais John Magufuli  februari 11, katika uzinduzi wa ofisi za mkurugenzi wa wilaya pamoja na hospitali ya wilaya hiyo.

Leo Jumatatu Februari 17 Waziri Lukuvi ameambatana na katibu mkuu wa wizara hiyo Merry Mkondo wamekabidhi ekari hizo kwa viongozi wa wilaya na manispaa ya kigamboni akiwemo mkuu wa wilaya hiyo Sara Msafiri.

”Leo nimetimiza maagizo ya Rais Magufuli ya kukabidhi ekari 715 mbele ya uongozi wa manispaa na wilaya ya Kigamboni natarajia kuona maeneo haya yanakuwa ya umma na sio kiwanja au makazi ya mtu mmoja mmoja”

Naye Mkuu wa wilaya hiyo Sara Msafiri amemshukuru waziri Lukuvi kwa kutimiza ahadi na kuahidi kushirikiana na wizara hiyo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.

 

Mwiko wanufaika wa Tasaf kuchangia miradi ya maendeleo
Rapa 50 Cent amkana French Montana