Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Likuvi ameeleza jinsi Ofisa Mikopo wa Benki moja Jijini Dar es Salaam, alivyojipatia nyumba tano kutokana na kudhulumu wateja.

Alisema, kuna baadhi ya Benki kwa kushirikiana na adalali, matapeli wanawaibia Wananchi na kuuza nyumba zao kwa mnada pasipo kufuata taratibu.

Amesema maofisa hao wanapotoa mikopo kwa wateja wao, wanasubiri ndani ya mwaka mmoja kisha wanafuata madalali ambao wanakwenda kupiga mnada mali iliyowekwa dhamana kwa madai ya kushindwa kulipa deni.

Dar: Abiria wa mwendokasi wabadilishiwa njia

“Watu hawa maskini wanakopa kwa ajili ya kuhakikisha wanapata angalau nyumba za kuishi, inapotumika hila ili kumfilisi kwa kuchukua nyumba yake haikubaliki kamwe,” amesema Waziri Lukuvi.

Haya ni baadhi ya maeneo yaliyoathirika na mvua za leo

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, Serikali imegundua jambo hilo na kuwaonya watu wanaondesha mtandao huo kuacha mara moja.

Tamko la TCRA siku nne kabla ya kufunga laini zisizosajiliwa
Dar: Abiria wa mwendokasi wabadilishiwa njia

Comments

comments