Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amekabidhi hatimiliki 88 kwa wakazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam kati ya 4333 ambazo ziko kwenye hatua za mwisho katika mradi wa urasimishaji wa makazi holela.

Amesema kuwa Serikali ya Aawamu ya Tano imedhamiria kurasimisha makazi nchi nzima ili kuongeza thamani ya ardhi au maeneo husika. huku akisema ardhi yenye hatimiliki thamani yake huongezeka kwani inatambuliwa na taasisi za fedha ambazo ni rahisi kukuopesha wenye hati.

“Kwa hati hizi zilizotolewa takribani 4333 tukisema kila nyumba ikopeshwe kwa kiwango cha chini cha shilingi milioni 10, kwa siku ya leo Kimara inapata mtaji wa karibu bilioni 40.5,”amesema, Lukuvi

Aidha, amesema kuwa maeneo yote ya miji ambayo hayajapimwa, yapimwe na halmashauri na manispaa zote nchini ili kuyaongezea thamani na kuondokana adha ya watu kujenga kwenye makazi holela.

Hata hivyo, Lukuvi ametoa onyo kali kwa matepeli wa ardhi kuacha vitendo hivyo mara moja kwani dawa yao ipo tayari na ameongeza kuwa madalali uchwara wa ardhi waache tabia ya kuwaonea wanyonge na kusababisha mali zao ziuzwe kwa njia ya udanganyifu.

 

Chadema watua kwa Kaimu Jaji Mkuu
Singida Utd Wafunga Dirisha La Usajili Kwa Kushusha Kifaa