Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya  Makazi, William Lukuvi amewatangazia kiama vigogo wanaomiliki majumba hapa nchini kwa kuwaeleza wazi kwamba wataumbuka kwa kutangazwa majina yao hadharani endapo hawatatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.

Aidha rungu hilo litawagusa pia wamiliki wengine wote wasiolipia kodi za ardhi na majengo yao nchini, hiyo ikimaanisha kwamba ni pamoja na wamiliki wa majumba ya kifahari katika maeneo ya Masaki, Msasani, Mbezi beach, Oysterbey, Tegeta na kwingineko jijini Dar es salaam.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Lukuvi amesema kuwa majina yatakayo wekwa hadharani yatakuwa halisi na wala hatajali kuwa ni ya kiongozi wa Serikali ama Kigogo yeyote ili mradi atakuwa amebainika kukwepa kulipa kodi.

“Wapo baadhi ya watu wanamiliki ardhi na majengo, lakini hawalipii kodi, nimesema Januari mwakani, majina yote nitayaweka hadharani na watapigwa penalti mara mbili yake na baada ya hapo watachukuliwa hatua nyingine za kisheria”amesema Lukuvi.

Pia amesema kuwa Serikali haitasita kuyafuta mashamba ambayo hayajaendelezwa ama kufuata utaratibu wa umiliki wake hata kama yalichukuliwa kwa mkopo benki.

Salum: Mfumo wa tume ya uchaguzi zanzibar (ZEC) uboreshwe
Ndege zisizo na rubani kuanza kutoa huduma za kiafya Tanzania