Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William lukuvi amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri, maofisa ardhi, ujenzi na mipango miji kuweka alama ya X kwenye nyumba zote zilizojengwa bila kufuata utaratibu.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, wakati akitatua mgogoro wa ardhi ambapo ameagiza shamba lililokuwa la mifugo la malonje wilayani humo lirudishwe Serikalini.

Amesema kuwa tatizo la ujenzi holela huanza pale wakurugenzi wa halmashauri, maafisa ardhi, ujenzi na mipango miji wanapoacha kutimiza wajibu na majukumu yao ya kufuatilia watu wanaojenga holela katika maeneo mbalimbali bila vibali.

“Hatuwezi kuendelea na urasimishaji wa makazi wakati chanzo cha tatizo hilo kinajulikana, kwa hiyo naagiza wakurugenzi wa halmashauri, maofisa ardhi, ujenzi na mipango miji kuweka alama ya X kwa majengo yote yanayojengwa bila vibali,”amesema Lukuvi

Hata hivyo, Lukuvi ameongeza kuwa atapambana na viongozi hao pale atakapokuta majengo ya mji yamejengwa sehemu ambayo haina kibali, hivyo kuwatahadharisha kufanyakazi kwa bidii

Video: Mtoto aliyefanyiwa oparesheni 10 tumboni amuomba Rais Magufuli, Waziri Ummy, Makonda kuokoa maisha yake
Wanafunzi 15 wafariki dunia baada ya mlipuko kutokea