Elizabeth Michael aka Lulu ametoa ufafanuzi kuhusu post yake iliyoenda viral muda mfupi kuhusu warembo wa Tanzania na nafasi ya ubunge wa viti maalum.

Muigizaji huyo wa ‘Foolish Age’, jana (July 12) alipost kwenye akaunti yake ya Twitter ujumbe unaowachana warembo wanaodhani kuwa muonekano wao wenye mvuto na samani za mwili wao vinaweza kuwa chanzo cha kupata nafasi ya ubunge wa viti maalum kiulaini.

Tweet ambayo aliifuta muda mfupi baadae huku baadhi wakidhani amempa makavu ‘mrembo fulani maarufu’. Hata hivyo tuliinyaka.

“Viti Maalum Kama naviona vya mootooo. Sura nzuri peleka reception, T*ko Peleka (…)hapa ni makaratasi yenye Pass,Pass Pass yataanza kuongea.” Ilisomeka tweet yake.

Lulu alilazimika kufafanua ujumbe huo tata alipofanya mahojiano na ‘The Playlist’ ya 100.5 Times Fm inayoongozwa na Lil Ommy.

“It was a joke, but sort of ukweli pia. Kwa sababu mara nyingi kumekuwa na dhana, watu wa nje wanachukulia kama vile viti maalum ni vya kupeana. Yaani ukiwa mtoto mzuri na nini unapewa kiti maalum, ukiwa na shape na nini unapewa kiti maalum,” alifunguka.

“So what I did ni kwamba, probably watu wanaweza kuichukulia vibaya… wameichukulia kama nimemsnitch mtu, I’m not like that na sinaga hayo mambo kabisa. Ni kwamba I made it as a joke, lakini watu wasichukulie poa kwamba kila anaewekwa pale… kwamba ana sura nzuri, kila anaewekwa pale ana umbo zuri.”

Dr. Slaa Abeza Nguvu Ya Magufuli Dhidi Ya Ukawa, ‘Hatuwezi’
UKAWA Wataja Tarehe Ya Kumtangaza Mgombea Wa Urais
Tags