Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Dar es salaam inatarajia kuanza kusikiliza ushahidi wa kesi ya mauaji bila kukusudia inayomkabili Msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael maarufu kama ‘Lulu’ Oktoba 19, 2017.

Lulu anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kumuua Msanii mwenzake Steven Kanumba bila kukusudia mnamo Aprili 7 mwaka 2012 nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican.

Baada ya kukamatwa na kuwekwa ndani alipandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo hakutakiwa kujibu kitu chochote, na baadae kesi iyo ilihamishiwa mahakama kuu ili kusikilizwa tena ambapo Lulu aliachiwa kwa dhamana mwaka 2013.

Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji ya bila kukusudia iliyotolewa na Mahakama Kuu, kesi ya Lulu itaanza kusikilizwa siku ya Oktoba 19/2017 mbele ya Jaji Sam Rumanyika.

 

 

Jamii yatahadharishwa kuhusu mafuriko
Mahakama Kuu Kenya yaondoa zuio la maandamano