Gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Prof. Florens Luoga leo ameanza rasmi kazi yake na kuchukua nafasi ya Benno Ndulu.

Ambapo ameahidi kufanya kazi na kurekebisha changamoto zinazoikabili sekta ya benki, na kusema kuwa jambo la kwanza atakalofanya ni kukutana na wadau wa sekta za mabenki ndani na nje ya nchi, ili kujadialiana mambo mbalimbali  na changamoto zinazoikabili sekta hiyo na kuhakikisha zinafanyiwa kazi.

Hata hivyo Prof.Luoga amesema tayari ameshakutana na Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango kama namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya wizara na mabenki.

Profesa Luoga alikuwa ni mwalimu wa sheria Chuo Kikuu Dar Es Salaam (UDSM) kabla ya kuteuliwa na Rais Magufuli tarehe 23, Oktoba 2017.

Moto walipuka Wodini, waua
Mabasi ya mikoani kufanya safari zake saa 24