Mchungaji Antony Lusekelo maarufu kama Mzee wa upako ameweka wazi juu ya upendo alionao kwa msanii Diamond Platinumz akidai kuwa ni mnyenyekevu huku akimponda vikali msanii Alikiba akidai kuwa anaringa na amezifananisha tabia hizo na mafanikio yao.

”Mimi nampenda sana Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu, simpendi Alikiba sababu ana kiburi, nadhani kwa sababu amekaa kariakoo. Ukimpiga simu Diamond anapokea kwa unyenyekevu ila Alikiba anapokea kwa maringo. Ndo maana Diamond amefika mbali” Amesema Lusekelo.

Amezungumza hayo leo pindi alipokuwa anafanya mahojiano na stesheni ya Redio ya TimesFM alipokwenda kutoa ushuhuda juu ya kumpigia simu msanii wa muziki Abubakar Shabaan Katwila maarufu kama Qchillah kumsihi asiachane na muziki kwani yeye ni moja kati ya mashabiki wake.

”Qchief ni kijana wangu nimempigia simu na kumwambia asiache muziki” Anthony Lusekelo.

Aidha kwa tuhuma inayomkabili Alikiba akidaiwa kuwa anaringa ameshalizungumzia swala hilo pindi alipofanya mahojiano na Radio ya Clouds FM wakati akifanya ziara ya kukitambulisha kinywaji chake cha Energy Drink ‘Mofaya’ ambapo alisema yeye haringi bali anajipenda kama ambavyo mtu anatakiwa kujipenda.

”Hayo ni maneno ya watu tu lakini lazima mfahamu kwamba mimi siwezi kuishi maisha ya kuigiza. Mimi niko real, siringi lakini najipenda kama amabvyo kila mtu anapaswa kujipenda. Naheshimu mkubwa na mdogo , wakati mwingine watu wanatengeneza maneneo tu”. amewahi kusema Alikiba

 

 

Hofu yatanda vitendo vya ulawiti kwa watoto wa kiume vyakithiri
Video: Makamba kukomesha matumizi ya Mkaa

Comments

comments