Mbunge wa Jimbo la Mtera kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Livingstone Lusinde amesema kuwa serikali imeshindwa kusimamia mambo yake vizuri jambo ambalo linapelekea matumizi ya fedha kuwa makubwa huku miradi ikikwama.

Ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kusema kuwa serikali imekuwa ikishindwa kusimamia vizuri matumizi ya fedha jambo ambalo linazidi kurudisha nyuma kimaendeleo.

Amesema kuwa wakati mwingine serikali inashindwa kusimamia matumizi mazuri ya fedha kwani ikisimamia vizuri fedha, thamani ya fedha itaonekana na upatikanaji wa maji utakuwa ni wa uhakika.

“Kwenye serikali imetolewa bilioni moja pale Kwayungu kwa ajili ya kujenga bwawa la umwagiliaji mpaka sasa bwawa halijakamilika, hakuna miundombinu na bilioni imeliwa kwa hiyo unaweza kuona matumizi mabaya kwenye miradi ya maji kwa upande wa serikali ndiyo yanatuletea matatizo makubwa,”amesema Lusinde

Hata hivyo, ameongeza kuwa WFP wametoa milioni mia saba tisini na tisa kwenye jimbo la Mtera kwa fedha hizo hizo wamepata matenki makubwa ya lita laki nane matatu, Visima kumi na nane, mashamba heka mia tatu kwa ajili ya umwagiliaji, visima kumi na mbili vilivyofungwa solar Power kwa ajili ya wananchi kupata maji, lakini kwa upande wa serikali hakuna kitu kilichofanyika.

 

 

Mwendokasi kuhamishiwa stendi ya mabasi Ubungo
Video: NBS yafunguka kuhusu mfumuko wa bei