Kocha mpya wa Yanga, George Lwandamina ametua Yanga na kukabidhiwa jukumu la kuitoa Yanga ilipofikia.

Lwandamina raia wa Zambia ametambulishwa leo rasmi na Makamu wa Rais wa Yanga, Clement Sanga mbele ya waandishi wa habari.

“Tunaamini kocha atatusaidia kutoka hapa tulipofikia na kusonga mbele hasa katika michuano ya kimataifa,” alisema.

Lwandamina atakuwa akifanya kazi na Hans van der Pluijm ambaye sasa ni mkurugenzi wa ufundi.

Pluijm ambaye amepanda cheo, aliifikisha Yanga kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.

Wakati huo huo Kocha George Lwandamina amesema atapambana vilivyo kuhakikisha anafanya vema huku akikiri kuwa na jukumu zito la kutetea ubingwa wa Tanzania bara.

“Lakini nitapambana kufanya vizuri, najua ni changamoto mpya kwangu lakini nitafanya kila linalowezekana,” alisema.

Hata hivyo Lwandamina ameomba Wanayanga kumpa ushirikiano ili kufikia malengo yake.

AVB Ajipa Matumaini Ya Kumnasa Mikel Obi
DK. Mpango: Uchumi wa Tanzania uko safi