Kocha Mkuu wa kikosi cha Azam FC, George Lwandamina amesema kuwa bado haridhishwi na nafasi waliopo, na watapambana kusaka nafasi ya kwanza kwenye misimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayokamatwa na Young Africans wenye alama 51.

Lwandamina ametoa kauli hiyo huku kikosi chake kikitoa kuigalagaza Mtibwa Sugar mabao 2-0, katika mchezo wa mzunguuko wa 25 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Akizungumzia mipango yao, kocha huyo kutoka nchini Zambia amesema: “Nafurahia kwa matokeo ya ushindi wa mabao 2-0 tulioupata dhidi ya Mtibwa Sugar, kama timu tunajua wazi kuwa matokeo yetu hayajawa ya kuridhisha sana msimu huu.

“Tumepata muda wa kurekebisha mapungufu tuliyokuwa nayo, na sasa tutahakikisha tunafanya vizuri zaidi ili kuweza kupanda juu zaidi kwenye msimamo, hatubweteki kwa na nafasi ya pili tuliyonayopo kwa kuwa tuna imani kuwa tunaweza kukwea juu zaidi kwenye msimamo.”

Kwa ushindi wa mabao 2-0, Azam FC imejisogeza hadi kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha alama 47, wakiwashusha mabingwa watetezi Simba SC wenye alama 46 katika nafasi ya tatu.

Aweso akiri miradi ya maji kutokutoa maji, awaonya Wakandarasi, Wahandisi
Mwinyi amfungukia Rais Samia, ‘ungekuwa wimbo ningesema urudiwe’