Kiungo wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Thadeo Lwanga amerejea nchini baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Lwanga amerejea Dar es salaam na kuanza Program maalum, tofauti na wachezaji wengine wa Simba SC waliobaki jijini humo, baada ya kuachwa kwenye safari ya Zambia.

Kiungo huyo anayepigiwa upatu wa kuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC wakati wa mchezo wa Kariakoo Dar Derby Jumamosi (Desemba 11), ana wakati mgumu wa kumshawishi Kocha Mkuu Pablo Franco Martin ambaye hajawahi kumuona tangu alipoanza kazi klabuni hapo.

Kwa sasa nafasi ya Lwanga kwenye kikosi cha Simba SC inatumikiwa na Kiungo Mtanzania Jonas Mkude, ambaye ameonekana kuaminiwa sana na Kocha huyo kutoka nchini Hispania.

Wakati huo huo kikosi cha Simba SC kimeendelea na maandalizi ya kuelekea mchezo dhidi ya Young Africans, kikiwa mjini Lusaka-Zambia, ambako kilikwenda kwa ajili ya mchezo wa Mkondo wa Pili wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Red Arrows.

Simba SC ilianza maandalizi hayo jana Jumatatu (Desemba 06), huku uongozi ukiamini mji wa Lusaka ni mahala sahihi kwa maandalizi ya kuwakabili Watani zao wa Jadi Young Africans Jumamosi (Desemba 11).

Moto walipuka Gerezani, wahofiwa kuua wafungwa
Geita Gold kumrudisha Haruna Niyonzima