Kundi la waasi wa M23 limesema halihusiki na tangazo la usitishwaji mapigano lililotolewa jijini Luanda nchini Angola, hivyo kutoa wito wa mazungumzo ya moja kwa moja na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC.

Msemaji wa M23 Lawrence Kanyuka, amesema wanaonya kupitia waraka wa mitandao ya kijamii na hakukuwa na mwakilishi wao kwenye mkutano wa kilele wa Luanda, hivyo maazimio yake hayawahusu.

Mmoja wa wapiganaji wa kikundi cha waasi cha M23. Picha ya The Independent Uganda.

Rais wa DRC, Felix Tshisekedi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Vincent Biruta walihudhuria mkutano huo mdogo wa kilele mapema Jumatano Novemba 23, 2022 uliowataka waasi kusitisha mapigano kufikia hii leo jioni Novemba 25, 2022.

Katika kikao hicho, wajumbe waliwataka M23 kujiondoa kwenye maeneo yote wanayoyashikilia na kurejea kwenye maeneo yao ya awali na endapo watakataa kuondoka, kikosi cha Afrika Mashariki kinachopelekwa mjini Goma kitatumia nguvu dhidi yao.

Neymar azua hofu kambini Brazil
Ahmed Ally afunguka mazito Simba SC