Wakati majaribio ya kurejesha amani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ya viongozi wa kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yakiendelea, waasi wa Vuguvugu la Machi 23 wamesonga mbele kuteka maeneo ya mashariki mwa DRC.

Serikali ya Kongo, bado inadai Rwanda inaandaa mapigano kati ya nchi hizo mbili kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 na hapo jana Rais wa Kenya, William Roto alitarajiwa kufika DRC ili kuzungumzia hatua za amani kati ya pande mbili zinazopingana.

Wapiganaji wa M23 nchini DRC. Picha ya iNews

Katika miezi michache iliyopita, watu wengi wa Kinyarwanda wanaozungumza Kikongo wakijulikana kama Banyamurenge na Watutsi wametangazwa kuuawa nchini DRC, kwa kushukiwa kuwa ni washirika wa M23.

Wakati waasi wa M23 wakisonga mbele kudhibiti maeneo zaidi mashariki mwa DRC, zaidi ya wakimbizi 89 wamevuka mpaka wa Kabuhanga kutafuta hifadhi nchini Rwandaambayo inakanusha kuwaunga mkono waasi hao wa M23.

Kocha N'diaye aondoka Horoya AC
Polisi wadaiwa kuficha tukio la ubakaji