Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni amesema Baraza la Taifa la Usalama Barabarani limeifuta wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyokuwa ikifanyika kila mwaka kwa madai imekuwa ikitumia gharama kubwa huku ajali zikiendelea kuwepo.

Akizungumza na wajumbe wa baraza hilo Jijini Dodoma wakiwemo wakuu wa vikosi vya Usalama Barabarani wa Mikoa yote bara na Visiwani, ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza hilo amesema baraza limefikia uamuzi huo kutokana na kushindwa kufikia malengo pamoja na kumvua madaraka mwenyekiti wa baraza hilo mkoa wa Mbeya Chacha Mugaka.

Naye mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini, Fortunatus Muslim amesema kutokana na oparesheni nyakuanyakua iliyofanyika kwa madereva wa magari kufanikiwa wanapanga kuihamishia kwa madereva wa bodaboda  na kudai wamekuwa kikwazo kikubwa na kusababisha ajali nchini.

Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliamo, Elias Kwandikwa amesema wizara hiyo imejipanga katika kuhakikisha inaondoa changamoto za sekta ya usafiri ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara.

Sababu ya 50 Cent kununua tiketi 200 kwenye shoo ya Ja Rule
Bunge lasitisha kufanya kazi na CAG, ‘yaani atuite kama mazezeta..!’