Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) kwa kushirikiana na UN-Women pamoja na Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) wanatarajia kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kitaifa.
 Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa WiLDAF Dkt. Judith  Odunga wakati wa mkutano  na  waandishi wa habari ambapo alisema kuwa maadhimisho hayo yanayotarajia kuanza tarehe 25 Novemba na kufikia kilele chake Desemba 10 mwaka huu.
 Maadhimisho hayo yana lengo la kutoa elimu na kuhamasisha Umma kupinga ukatili wa kijinsia na kuhimiza umuhimu wa elimu salama kwa wote.
 “Ndani ya siku hizi, kuna siku nyingine muhimu za kimataifa kama vile Novemba 25 ni siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake, Novemba 29 ni siku ya kimataifa ya watetezi wa Haki za Binadamu na  Desemba 1 ni siku ya Ukimwi Duniani, alisema Odunga.
 Odunga alisema kuwa siku hizo 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni tukio la kimataifa la kila mwaka ambalo lina lengo la  kuwa na nguvu  ya pamoja katika kuzuia  kuenea kwa janga hilo.
 Amesema kuwa tukio hilo hapa nchini linatarajia kufanyika kitaifa katika kanda tano, ambazo ni Kanda ya Mashariki na Dar es Salaam, Kanda ya Kati Dodoma, Kaskazini, Kusini na Kanda ya ziwa.
Katika kila kanda kutakuwa na shughuli mbalimbali kama vile midahalo ambayo italeta chachu ya mabadiliko katika nchi pamoja na  maandamano ya amani.
 Kwa upande wake Afisa wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia Mkoa wa Kipolisi wa Ilala  Christina Onyango amesema kuwa maadhimisho hayo yamesaidia kuongeza uelewa kwa jamii , hatua ambayo imesaidia kupokelewa kwa kesi nyingi za ubakaji ukilinganisha kwa miaka ya nyuma.
 Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ni anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora . Angelah Kairuki.
 Kauli mbiu ya maadhinmisho ya mwaka huu ni funguka!pinga ukatii wa kijinsia: elimu salama kwa wote.

Makonda: Sitaki watumishi mizigo katika mkoa wangu
Hillary Clinton aponea chupuchupu kwenye mikono ya Donald Trump